Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa hadhrat Ayatollah Nouri Hamedani kufuatia kuuawa kishahidi Sardar Luteni Jenerali Mujahid Ali Shadmani, ni kama ifuatavyo:
Bismillahir Rahmanir Rahim
Katika siku hizi za maombolezo ya Bwana na Kiongozi wa Mashahidi, Abā ‘Abdillah al-Husain (aa), ninatoa pongezi na rambirambi kwa wananchi wote wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hususan kwa watu wa Hamadan – mji wa mashahidi na watu waumini – kutokana na mnasaba wa kuuawa kishahidi kwa ndugu mpenzi, mkweli na mujahid, Sardar Luteni Jenerali Bwana Ali Shadmani.
Bila shaka, damu ya shahidi huyu na mashahidi wengine wapendwa itakuwa na athari kubwa katika kuangamiza utawala dhalimu na haramu wa Kizayuni.
Wananchi wapendwa, na wanamapinduzi wenye kusubiri wa Iran, kwa mshikamano na umoja waliouonyesha hadi leo, wataiendeleza njia hii, na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Imam wa Zama (aj) pamoja na uongozi wa Kiongozi mpendwa, ushindi kamili utapatikana in shaa Allah.
Kuhudhuria kwa wapendwa wote katika mazishi ya wapendwa hawa litakuwa ni jibu thabiti kwa porojo na maneno ya kipuuzi ya viongozi wenye kutakabar.
6 Tir 1404 (Hijria Shamsiyya)
Hussein Nouri Hamedani
Maoni yako